THE REGISTERED TRUSTEES OF MAAHAD SHAMSIL MAARIF ISLAMIYYAH, NO. 2072.

Latest News

Contact Info

Lengo na Maono

Malengo ya Muda Mrefu

Taasisi hii ina malengo makuu manne na hayo ni kama ifuatavyo:

  1. Kufundisha/kuhisha elimu ya dini ya Kiislamu na kuiweka katika jamii ya Kiislamu.
  2. Kuandaa walimu wa dini ya Kiislamu wenye ustadi wa kufundisha katika daraja tofauti za kimasomo.
  3. Kuwalea na kuwakuza vijana wa Kiislamu katika malezi na tabia bora, ambazo ndiyo njia tulizoachiwa na wasisi wetu.
  4. Kuwafundisha vijana umuhimu wa kulinda, kuheshimu, na kuendeleza Amani iliyopo ndani ya taasisi, katika jamii na nchi nzima kwa ujumla.

Ili kuweza kutimiza malengo hayo, taasisi inajikuta inatakiwa kuweza kujikwamua kiuchumi katika kuboresha malengo yake. Kwa sasa makao makuu ya taasisi pekee kuna wanafunzi 939. Pia, kutokana na sadaka chache tunazozipokea kutoka kwa walimu na viongozi, wanalazimika kufanya kazi za kujitolea kwa asilimia 80%. Hivyo, tunaomba kupata Waislamu watakaojitolea kusaidia gharama za kuendesha taasisi, kama vile posho za walimu, viongozi, vitendea kazi vya ofisi (stationery), na mahitaji mengine mbalimbali. Gharama hizi hazijaweza kuzipanga kwa sababu hatuna wafadhili wa kuzilipa.

Kutokana na wanafunzi wanaokuja kusoma katika taasisi yetu, wengi wao familia zao hazina uwezo. Hivyo, taasisi haiwatozi ada ya malipo kwa wanafunzi hao. Hii imekuwa changamoto kwa taasisi kuweza kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi wao.

Taasisi pia inakabiliana na changamoto zifuatazo:

  1. Hakuna mabweni ya kulala wanafunzi; vyumba vilivyopo sasa havikidhi mahitaji husika.
  2. Upungufu wa madarasa ya kusomea wanafunzi.
  3. Kukosekana kwa posho za kujikimu kwa walimu.
  4. Kutokuepo kwa chakula kwa wanafunzi; kwa sasa wanajisaidia wenyewe, jambo ambalo lipo nje ya uwezo wao.
  5. Uchakavu wa majengo yaliyopo sasa, ikiwa ni pamoja na msikiti, yanahitaji ukarabati wa haraka ili kuzuia uchakavu huo usiendelee.

Taasisi ina matarajio ya kuwa na uwezo wa kiuchumi ili kukidhi mahitaji yake, kutatua changamoto zilizopo, na kupokea wanafunzi wengi zaidi.

Malengo ya Muda Mfupi

Malengo ya muda mfupi kwa taasisi ni haya yafuatayo:

  1. Kufundisha vijana wa Kiislamu, wanaume na wanawake, kila siku.
  2. Kusimamia na kuhakikisha kuwa matawi yake yote yasiyopungua 100 yanaendelea kupata elimu kwa kiwango kinachostahiki, kidhamu, na ufanisi/uelewa ulio bora zaidi.
  3. Kuzalisha waalimu wengi zaidi ili kuweza kufikia malengo ya kueneza elimu ya dini ya Kiislamu ndani na nje ya nchi.

 

Mahusiano

Taasisi hii ni ya kidini ina heshimu na kutii mamlaka za kiutawala zilizopo na itaendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa sharia zilizowekwa pamoja na kuheshimu katiba ya jamhuri ya muunganao wa Tanzania. Pia ina mahusiano mazuri na kushirikiana na taasisi nyingine za kidini na zisizo za kidini maadam jazivunji amani iliyopo katika taasisi, jamii na nchi kwa ujumla na haziendi kinyume na sharia ya dini na sharia ya nchi.Pia inaheshimu pamoja na kuishi vyema na jamii kwa mujibu wa sheria zilizopo na kutovunja sharia za nchi

Anuani

MAAHAD SHAMSIL MAARIFIL ISLAMIYYAH

P.O. BOX 1784

TANGA-TANZANIA