THE REGISTERED TRUSTEES OF MAAHAD SHAMSIL MAARIF ISLAMIYYAH, NO. 2072.

Latest News

Contact Info

Historia ya Taasisi na Matawi yake

Karibu...

Maahad Shamsil Maarifil Islamiyyah

Madrasa ya Shamsil Maarifil Isamiyyah ilianzishwa katika mtaa wa Majengo mnamo tarehe 10/04/2000 na aliyekuwa kiongozi wake mkuu wa wakati huo , Al-Marhum Al-Aalim Allamah Sheikh Muhamadi ibin Aboubakry Al-Burhaan, Allah amrehemu, akishirikiana na wanafunzi wake wakiongozwa na Sheikh Samir ibin Sadick Hemedi, aliyekuwa ni makamu (Naibu) wake wakiungwa mkono na Waislamu wa eneo la Majengo pamoja na Waislamu kutoka maeneo mbalimbali, wanaume na wanawake.

Taasisi ya Maahad Shamsil Maarifa Islamiyyah ilianza rasmi kazi zake za kusomesha elimu ya dini ya Kiislamu tangu tarehe 10/04/2000 kabla ya kusajiliwa kuwa taasisi rasmi katika eneo la Majengo.

Madrasa hii ilisajiliwa rasmi kuwa taasisi kamili kwa jina "The Registered Trustees Shamsili Maarifu". Namba yake ya usajili ni 2072.

Kwa sasa taasisi hii ipo mtaa wa Magomeni B, kata ya Duga, tarafa ya Pongwe, jiji la Tanga, Tanzania. Taasisi kwa sasa ina vyumba nane (8) vya madarasa vinavyotumika; hata hivyo, kuna Waislamu waliojitolea kujenga vyumba (10) vya madarasa ambavyo vipo katika hatua ya mwisho kukamilika. Iwapo vitakamilika, taasisi itakuwa na vyumba kumi na nane (18) vya madarasa kutokana na idadi ya wanafunzi wote miatisa thelathini na tisa (939) waliopo. Kwa wastani wa kila chumba cha darasa, wanafunzi arubaini (40), tunapata mapungufu ya vyumba vya madarasa sita (6). Hilo ndilo hitaji la taasisi kwa sasa.

Pia taasisi hii inasimamia matawi yake yasiyopungua mia moja (100) yaliyopo maeneo mbalimbali, hivyo kupelekea idadi ya wanafunzi wote, wale wa makao makuu na matawi, kufikia wanafunzi wasiopungua elfu nane (8000).

Mawasiliano

Mudir (Mkuu wa Chuo):
Sheikh Samir Sadick Hemed
Simu: +255 754743537/+255 620143147

Naibu (Makamu Mkuu wa Chuo):
Sheikh Rashid Ally
Mob: +255 563645535

Mwenyekiti:
Hon. Waziri Hassan
Simu: +255 713771263

Katibu:
Ustadh Umar Athumani
Simu: +255 627755199